Nabii Dkt.Mjuni awauma sikio watumishi wa Mungu

NA DIRAMAKINI

MTUMISHI wa Mungu wa Huduma ya Yerusalemu Pomerini Ministry iliyopo Kilolo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Nabii Dkt.Mjuni Kisha amesema,watumishi wa Mungu wana nafasi kubwa ya kuchochea vipawa vya wasaidizi wao ili waweze kutimiza kusudi la Mungu lililowekwa ndani yao.

Nabii Dkt.Mjuni amefafanua kuwa,ni muhimu kufahamu kuwa kila mwanadamu amezaliwa akiwa na kusudi fulani au wajibu fulani wa kuutimiza ulioko ndani yake, na katika wajibu huo ili aweze kuutimiza ipasavyo, Mungu huweka karama au kipawa kwa ajili ya kumuwezesha mtu huyo kulitimiza kusudi hilo.

"Watumishi wa Mungu tusifanyie kamari kwenye vipawa vya watu,mgonjwa akifika akaombewa na wahudumu akapona tuwambie watu kwamba wao ndio waliofanya kazi kubwa kuliko kuwatumia wao kufungua watu kwa ajili ya kutangaza jina lako,"amefafanua Nabii Dkt.Mjuni.

Amefafanua kuwa,karama au kipawa kinapokuwa ndani ya mtu kuna mambo kadhaa yanayopaswa kufanyika ili kiweze kukua au kukomaa au kujitokeza katika ubora wake, suala hilo sio lingine ni kuchochea kipawa hicho kilichomo ndani ya mtu aliyekusudiwa na Mungu kutumiwa katika shughuli husika.

Pia, Dkt.Mjuni amewashauri watumishi wa Mungu kuendelea kutambua mchango na vipawa vya wazee na walezi wa huduma zao.

"Pili tutambue mchango na vipawa vya wazee wetu wa huduma,tatu tuhubiri pia mazuri yanayofanywa na nchi yetu kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan,tusitafute huruma za watu kwa kutokuwa wazalendo wa nchi yetu,nchi yetu ina matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kupitia maombi na kuheshimu mamlaka, kwani mamlaka hutoka na kuwekwa na Mungu,"amefafanua Nabii Dkt.Mjuni.

Nabii Dkt.Mjuni amerejea maandiko katika Biblia Takatifu, kitabu cha Warumi 13:1-2..."Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu;nao washindanao watajipatia hukumu."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news