Rais Dkt.Samia awapa zawadi ya Pasaka wana Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amewakumbuka wananchi wa Kata ya Tegeruka na Mgango Katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara waliokuwa wameachwa kwenye mradi mkubwa wa maji ya bomba wa Mugango- Kiabakari-Butiama unaogharimu shilingi Bilioni 70.5, ambapo ametoa shilingi Bilioni 4.75 za kujengewa miundombinu ya usambazaji wa maji kwenye kata hizo.

"Tunaanza kwa kutoa shukrani nyingi sana kwa Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Kata zilizokuwa zimeachwa kwenye mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 70.5 ya Maji ya Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama, sasa zimepatiwa fedha shilingi Bilioni 4.75 za kujengewa miundombinu ya usambazaji wa maji kwenye kata hizo,"imeeleza sehemu ya taarifa ya iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 6, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara ambapo taarifa hiyo imesema kuwa wananchi wamepokea kwa shukurani na kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo wakisema ni 'zawadi ya Pasaka kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali.

"Kwa hiyo, wananchi waishio penye chanzo cha maji (Kata ya Mugango yenye vijiji 3) ya Bomba hili, na wananchi waishio kwenye njia ya bomba hili (Kata ya Tegeruka yenye vijiji 3), na wao watapata maji kutoka kwenye Bomba hili hili hawajaachwa,"imeeleza taarifa hiyo;

UWEKAJI SAINI WA MRADI WA TEGERUKA- MUGANGO

Mkandarasi wa Mradi huu wa kata mbili, ameishapatikana na taratibu zote zimekamilika, kifuatacho ni uwekaji wa saini katika Kijiji cha Mayano siku ya Jumatano ya Aprili 12,2023, saa 4 asubuhi, na wahusika watawekeana saini ya utekelezaji wa Mradi huo Kijijini Mayani, Kata ya Tegeruka.

"Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali watakuwepo kushuhudia tukio hili la muhimu sana sana, karibuni kijijini Mayani tarehe 12 Aprili, 2023," imesema taarifa hiyo.

Naomy Fabian ni mkazi wa Tegeruka akizungumza na DIRAMAKINI amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya maji ambapo amesema uongozi wake tangu aingie madarakani umeleta neema kwa wananchi wengi hasa katika kuimarisha huduma za kijamii.

"Rais katupa zawadi ya Pasaka kwa kitendo hicho, kweli kinamama lazima tumpongeze Rais wetu kwa kutujali maji yanapokuwa karibu na tunapoyapata kwa wepesi inatupa faraja na kutiwezesha kufanya kazi za maendeleo tulidhani tumeachwa. Hongera pia kwa Mbunge wetu kufiatilia jambo hili kwa kweli Mungu ambariki sana Prof.Muhongo ma Rais Samia,"amesema Nyafuru Jackson.

Naye Mathias Shadrack amesema Uongozi wa Rais Dkt.Samia unaendelea kugusa moja kwa moja mahitaji ya wanananchi ambapo amesema dhamira yake ya kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi ina manufaa makubwa ikiwemo kuondoa usumbufu wa kutafuta maji kwa kina mama na mabinti na pia itaimarisha mahusiano ya ndoa na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news