Rais Kagame ahitimisha ziara ya kikazi nchini

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania na kurejea nchini Rwanda.
Mheshimiwa Kagame ameagwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ambaye aliambatana na; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye.

Viongozi wengine waandamizi wa Serikali waliomsindikiza ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz.
Akiwa nchini Rais Kagame pamoja na mweyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan walikubaliana kuimarisha masuala mbalimbali ya ushirikiano hususan biashara, miundombinu ya bandari, mradi wa umeme wa Rusumo pamoja na masuala ya ulinzi na usalama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news