SUZA wapongezwa kwa tafiti mbalimbali za afya

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Kinga na Elimu ya Afya, Dkt.Salum Slim Mohammed ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kwa kuendelea kufanya tafiti mbalimbali za afya ambazo zinasaidia wizara katika kuboresha afya nchini 
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya mradi wa Uimarishaji wa Huduma jumuishi za VVU, TB na Malaria wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua kwa baadhi ya wakuu wa vituo vya afya vya Unguja na Pemba.
Naye Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar, Dkt Salma Mahmoud Abdi amesema mradi huu utasaidia kupunguza vifo vya mama na watoto na kusaidia kuzuia msongo wa mawazo kwa wazazi waliojifungua.

Mradi huu umefadhiliwa na Global Fund kwa kushirikiana na Liverpool School of Tropical Medicine cha nchini Uingereza pamoja na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news