TANZANIA NA SCJohnson ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA KUPAMBANA NA MALARIA

NA MWANDISHI WAF

WAZIRI wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu leo Aprili 2,2023 amesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana na Kampuni ya SCJohnson ya nchini Marekani katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.
Tukio hilo limehudhuriwa na Makamu wa Rais Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Mark Martin, Balozi wa Umoja wa Viongozi wa nchi za Afrika dhidi ya Malaria (ALMA) Mhe. Anthony Okara pamoja na Mwenyekiti Mteule wa Baraza la Kutokomeza Malaria Tanzania Mhandisi Leodgar Tenga.
Tamko hilo limefikiwa kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyoifanya kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Racine, Winscosin nchini Marekani mwezi Mei, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news