WALIVYOSEMA WAWEKEZAJI KUHUSU MIRADI YA KIMKAKATI NCHINI

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI tatu za uchimbaji madini kutoka nchini Australia zilisaini Hati ya Makubaliano ya Mikataba ya Uchimbaji Madini ya Kinywa na Rare Earth Elements katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma ambapo miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Morogoro, Lindi na Songwe.
Wakizungumza katika hafla hiyo Watendaji Wakuu wa Kampuni ya Evolution Energy Ltd, EcoGraf Ltd na Peak Rare Earths Ltd walieleza kuhusu utekelezaji wa miradi yao nchini ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ameshuhudia tukio hilo Ikulu Chamwino jijini Dodoma. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Evolution Energy Ltd Phil Hoskins inayotarajia kuchimba madini ya Kinywe katika eneo la Chilalo wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi alisema anaamini mikataba iliyosainiwa italeta maendeleo kwa pande zote mbili.

Aidha, Hoskins amesema mkataba uliyosainiwa na Kampuni yake ni ya ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni hiyo ambayo itachangia maendeleo katika wilaya ya Ruangwa na Taifa kwa ujumla.
Pia, Hoskins amesema Kampuni ya Evolution Energy Ltd itaendelea kufanya tafiti katika mradi wa Chilalo kwa lengo la kuongeza Maisha ya mradi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Hoskins amesema jumla ya uwekezaji wa awali katika mradi wa Chilalo ni Dola za Marekani 100 ambapo mradi unatarajiwa kuajiri zaidi ya watanzania 100 katika hatua ya ujenzi wa mradi huo.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya EcoGraf Ltd Andrew Spinks inayotarajiwa kuchimba madini ya Kinywe katika eneo la Epanko wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro alisema, katika hatua ya awali kampuni hiyo imepanga kuwekeza jumla ya Dola za Marekani Milioni 127.7 na kutoa hisa kwa serikali ya asilimia 16 zisizofifishwa na kampuni hiyo kumiliki hisa za asilimia 84. 
Pia, Mwenyekiti wa Kampuni ya Peak Rare Earths Ltd Russel Scrimshaw inayotajia kuanza uchimbaji wa madini ya Rare Earth Element katika mradi wa Ngualla uliopo wilaya ya Songwe mkaoni Songwe alisema, Rare Earth ni madini muhimu na ni madini ya kimkakati ambayo yanatumika kutengeneza betri za magari ya umeme na matumizi mengine ya teknolojia ya kisasa.

Katika hatua nyingine, Scrimshaw alisema mradi wa Ngualla unatarajiwa kuajiri zaidi ya watanzania 300 katika kipindi cha ujenzi ambapo mradi una jumla ya uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani Milioni 437 na inatarajia kuwa na thamani za mauzo ghafi ya kiasi cha shilingi bilioni 1,860 baada ya kuanza uzalishaji 
"Tunaposhuhudia mikataba ya miradi mbalimbali ya madini ikisainiwa ni kielelezo kwamba nchi imefunguka kiuchumi na kisiasa ambapo taifa linashuhudia wawekezaji wanamiminika nchini kitu ambacho kinaonesha uongozi na usimamizi bora wa maelekezo ya Rais Samia katika Sekta ya Madini,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news