Watu 57 wanusurika kifo kwa ajali ya basi Kigali

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi nchini Rwanda (RNP) limeanza uchunguzi kuhusu chanzo cha moto ulioteketeza basi la uchukuzi wa umma la Kampuni ya Rwanda Interlink Transport Company (RITCO).

Kwa mujibu wa msemaji wa RNP katika Jimbo la Kusini, CIP Emmanuel Habyaremye, basi hilo lilishika moto majira ya saa kumi na mbili jioni Aprili 29,2023 katika Wilaya ya Kamonyi likitokea Kigali kuelekea Ngororero.

"Watu wote 57 waliokuwa ndani ya basi hilo wamenusurika kifo. RNP iliingilia kati na kuzima moto, lakini basi hilo lilikuwa limeharibika sana.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, lakini uchunguzi wa tukio hilo umeanza,"amesema CIP Emmanuel.

RITCO ni kampuni ya umma yenye ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ambayo ilianzishwa mwaka 2016 na ilizinduliwa rasmi Februari 6, 2017 ili kutoa suluhisho endelevu juu ya matatizo ya usafiri wa umma yanayoongezeka kwa wakazi wa vijijini, mijini na kanda nchini humo.(The New Times)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news