Wydad SC yaiondoa Simba SC katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika

NA DIRAMAKINI

LICHA ya Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam kuonesha ubabe katika dimba la ugenini la Mohamed wa V dhidi ya wenyeji Klabu ya Wydad Casablanca nchini Morocco wametolewa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kupitia mchezo wa marudio.

Katika kipindi cha kwanza cha mtanange huo ambao umeanza saa 4 usiku ya Aprili 28, 2023 ndani ya dakika ya 24 mchezaji Bouly Junior Sambou wa Wydad SC alizifumania nyavu za wageni wao Simba SC.

Bao ambalo lilidumu hadi dakika tisini za mtanange huo ambao licha ya Simba SC kuonesha ukomavu na utulivu katika mtanange huo, pia mambo hayakwenda vema.

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ambaye hakufanya mabadiliko yoyote ya kikosi kilichoibuka na ushindi wa bao moja kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, ilionekana mipangilio yake ilikua na malengo mazuri na kikosi kimefanya kazi ya kishujaa.

Baada ya dakika tisini kutamatika, miamba hiyo ya soka barani Afrika imepiga matuta ambao Simba SC imeambulia matuta matatu huku wenyeji wakishinda matuta yote (3-5)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news