Wydad SC yawatangulia Simba SC kwa bao

NA DIRAMAKINI

NDANI ya dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza katika Uwanja wa Mohamed wa V wenyeji Klabu ya Wydad Casablanca nchini Morocco katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika inaongoza kwa bao moja.

Ni bao lililopatikana baada ya Bouly Junior Sambou wa Wydad SC kuzifumania nyavu za wageni wao Simba SC kutoka jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mechi hii imeanzasaa nne usiku leo Aprili 28,2023 ambapo kwa upande wa Simba SC, Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ hajafanya mabadiliko yoyote ya kikosi kilichoibuka na ushindi wa bao moja kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news