Bado alama tatu, Yanga SC bingwa

NA DIRAMAKINI

YANGA SC ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara wamebakiza alama tatu tu kutawazwa kuwa mabingwa tena wa ligi hiyo kwa msimu wa pili mfululizo.

Ni baada ya ushindi mnono walioupata Mei 4, 2023 wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Stephanie Aziz Ki dakika ya 15 na Clement Francis Mzize dakika ya 21 dhidi ya wenyeji Singida Big Stars katika Uwanja wa LITI mjini Singida.

Kwa matokeo hayo Yanga SC inafikisha alama 71 na kuendelea kuongoza ligi kwa alama saba zaidi ya watani wao, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 27 kuelekea mechi tatu za mwisho.

Wakati huo huo, Singida Big Stars inabaki na alama zake 51 katika nafasi ya nne ikizidiwa alama mbili na Azam FC walio nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 27.

Awali, Simba SC walilazimishwa sare ya bao moja kwa moja na Namungo FC katika dimba la Majaliwa lililopo Ruangwa mkoani Lindi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news