Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kushiriki Maonesho ya NACTVET jijini Arusha

NA DIRAMAKINI

CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimebainisha kuwa, kitashiriki katika Maonesho ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) yanayotarajiwa kufanyika jijini Arusha.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa leo Mei 13, 2023 na Dkt.Mohamed Omary Maguo, Mhadhiri Mwandamizi na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

"Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kinapenda kuutarifu umma kwamba, OUT itashiriki katika maonesho ya NACTVET yanayotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Mei 16 hadi 22, 2023 katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

"Hivyo, tunawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani kutembelea maonesho hayo kwa ajili ya kujifunza na kujionea huduma na programu mbalimbali za masomo zinazotolewa na OUT,"amefafanua Dkt.Maguo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news