Dkt.Mwinyi akagua mali za CCM

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kwani Zanzibar wakati wa ziara yake kukagua mali za CCM katika maeneo mbalimbali ya Unguja leo Mei 7,2023, akiwa katika eneo la Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu).
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya michoro ya Jengo la Uwekezaji la Chama Cha Mapinduzi katika eneo la Kijangwani katika nyumba ilikozaliwa Chama cha Shirazi Association, wengine ni Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Fedha na Uchumi Zanzibar, Afadhali Taibu Afadhali (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Dimwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa, akiwa katika ziara yake kukagua mali za CCM na kuimarisha chama.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ziara yake kutembelia mali za Cha Cha Mapinduzi (CCM) katika maeneo mbalimbali ya Unguja leo na kuimarisha chama, akitembelea eneo la CCM Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ziara yake kukagua mali za Chama Cha Mapinduzi katika maeneo mbalimbali ya Unguja yamo katika uwekezaji CCM Maisara Wilaya ya Mjini Unguja akizungumza na Meneja wa Hoteli ya Maisara Delux Lodge,Rumanyika Felician, wakati wa ziara yake leo na kulia kwa Rais ni Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Uchumi na Fedha Zanzibar,Afadhali Taibu Afadhali, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Uenezi na Itikadi Zanzibar,Khamis Mbeto Khamis na kushoto kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news