DUA NJEMA KWA YANGA

UTENZI wa dua njema kwa timu yetu ya Yanga katika mchezo wao wa fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho unaochezwa leo tarehe 28/05/2023 majira ya Saa Kumi Alasiri kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam dhidi ya USM Alger ya Algeria. 
Tunaiombea timu yetu Yanga kila la kheir na ushindi wa kishindo katika mchezo huo.

1
Tumeshika misahafu
Tukimuomba Raufu
Kwa umoja ja siafu
Yanga yetu ikashinde


2
Tunaomba na kusifu
Kwa Mungu mtukufu
Wape ari mara dufu
Yanga yetu Tanzania

3
Kwa moyo safi kunjufu
Ya Rabi muaminifu
Wape nguvu halafu
Utulivu waongeze

4
Siha njema uwaafu
Waondolee sumbufu
Wape pia changamfu
Yanga yetu Tanzania

5
Zawadi ya masurufu
Kwa Rais Mtiifu
Ni Yanga kwa usanifu
Kuirarua USM Alger

6
Rais Samia mwadilifu
Ahadize kamilifu
Na Yanga timu sufufu
"M" za mama mtachukuwa

7
Amina Rabi Amina
Dua kwako Maulana
Kwa wezo wako Rabana
Tanzania tutashinda

MTUNZI
Dkt. Mohamed Omary Maguo
Mhadhiri Mwandamizi
Mshairi wa Kisasa
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Arusha
28/05/2023

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news