IJP Camillus Wambura afanya mabadiliko kwa makamanda wa Polisi nchini

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IJP Camillius Wambura amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa kwa kuwahamisha na wengine kupangiwa majukumu mengine.

Mabadiliko hayo yamefanyika Mei, 15, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Jeshi hilo Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IJP Camillius Wambura.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, David A.Misime- SACP amesema katika mabadiliko hayo IGP Camillius Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Longinus Alexander Tibishibwamu (RPC) kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Nafasi ya ACP Longinus inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salum Ramadhani Morcase ambaye alikuwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Pia amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Geofrey Sarakikya kwenda Makao makuu ya Polisi Dodoma.

Nafasi ya Sarakikya inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Michael Njera ambaye alikuwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi amesema aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Hamis Issah amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelekezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Makuri Imori.

David amesema aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu amehamishiwa mkoa wa Kagera kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Willium Mwampagale amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news