JKCI yaendelea kuwa baraka kwa mamia ya watoto wenye matatizo ya moyo

NA MWANDISHI WETU
JKCI

WATOTO 334 wenye matatizo ya matundu kwenye moyo, matatizo ya mishipa ya damu na valve za moyo wamefanyiwa uchunguzi na upasuaji katika kambi maalum ya ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza wakifanya upasuaji wa kuziba tundu la moyo wa mtoto wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upasuaji wa moyo inayofanyika katika taasisi hiyo.
Kambi ilianza tarehe 12/05/2023 na inatarajia kumalizika tarehe 19/05/2023 inafanywa na wataalamu wa magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza wakizima tundu la moyo wa mtoto wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upasuaji wa moyo inayofanyika katika taasisi hiyo. 

Kwa muda wa siku mbili tangu kambi hiyo ianze watoto 307 wamefanyiwa uchunguzi wa moyo ambapo kati yao watoto 19 wamefanyiwa upasuaji kwa njia ya tundu dogo ambao unafanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab na watoto nane wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news