Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa JNHPP yatoa wito,ujenzi wafikia asilimia 86.8

NA ZUENA MSUYA
Pwani

KAMATI ya Usimamizi wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere imetoa wito kwa watanzania kuendelea kuunga mkono utekelezaji wa mradi huo kwa kuwa una faida kubwa kwa nchi yetu na watanzania wenyewe.
Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Kufua umeme wa Julius Nyerere, Mei 14, 2023 mkoani Pwani.Wa nane kulia ni Mwenyekiti ya Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz na kushoto kwakwe ni Katibu wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti ya Kamati ya Usimamizi wa mradi huo ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, Mei 14, 2023 mkoani Pwani.

Ziara hiyo imehusisha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali zinazohusika moja kwa moja katika utekelezaji wa mradi huo, Kamishna wa umeme na Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati(CERE), Mhandisi Innocent Luoga pamoja na viongozi waandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Muonekano wa ujazo wa maji katika eneo la njia ya kupekela maji ya kuzungusha mitambo ya kuzalisha umeme wa Julius Nyerere, ilivyoonekana wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi huo ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi husika, Mei 14, 2023 mkoani Pwani.
Mwenyekiti ya Kamati ya Usimamizi wa Mradi huo ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz (kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere, Mei 14, 2023 mkoani Pwani.

Dkt. Yonaz amesema kuwa mara baada ya mradi huo kukamilika na kuanza kuzalisha umeme, mafanikio mengine makubwa yatapatikana katika sekta ya Uvuvi, Kilimo na Utalii na hivyo kukuza uchumi wa nchi na watanzania kwa jumla.
Vijana walioonekana wakiendelea na kazi katika nyumba ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme wa Julius Nyerere, wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi huo ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi husika, Mei 14, 2023 mkoani Pwani.

Aidha ameipongeza Wizara ya Nishati na TANESCO kwa kazi kubwa ya usimamizi na utekelezaji wa mradi huo kwa hatua iliyofikiwa ambayo inayotoa picha halisi kwa jamii, kuwa muda si mrefu umeme utaanza kuzalishwa.
Katibu wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba,(wa tatu kushoto) akiwaeleza jambo, Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo, Mei 14, 2023 mkoani Pwani.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alieleza kuwa hatua ya ujenzi wa mradi huo kwa sasa asilimia 86.8 kutoka asilimia 81.22 mwezi Desemba mwaka jana, kazi ya ujenzi inaendelea na matarajio ni kuanza kuzalisha umeme Juni 2014. 

“Maendeleo ya mradi ni mazuri sana ikilinganishwa na kipindi kile ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuja kuzindua rasmi zoezi la ujazaji maji katika bwawa hilo ambao eneo tulilokuwa tumekaa wakati ule kwa sasa limekuwa na maji yenye kina cha mita 30, kwa hiyo haiwezekani kufika pale tena, hiyo ni ishara inayoonesha maendeleo makubwa”, alisema Mhandisi Mramba.
Mhandisi Mkazi Lutengano Mwandambo (katikati) akiwaeleza jambo, Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo, Mei 14, 2023 mkoani Pwani.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha na maelekezo ambayo yamewezesha mradi huo kufikia hatua hiyo, wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Fedha wanaohakikisha malipo yanafanyika kwa wakati, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kusafirisha mitambo ya mradi huo.

Kamati hiyo imetembelea eneo la Kingo za Bwawa husika, Tuta kuu la Bwawa, nyumba ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme na njia ya kupeleka maji ya kuzungusha mitambo ya kuzalisha umeme, pamoja na eneo la ufungaji wa mitambo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news