Kocha Ulimboka Alfred Mwakingwe, Yusuph Kitumbo wafungiwa maisha

NA DIRAMAKINI

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imewafungia maisha Kocha Ulimboka Alfred Mwakingwe na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tabora (TAREFA), Yusuph Kitumbo wasijijusishe na soka.

Ulimboka, nyota aliyeisaidia Simba SC kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003 kwa kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Zamalek ya Misri - anatuhumiwa kushiriki mpango wa upangwaji matokeo ya mechi.

Hayo ni kwa mujibu w ataarifa iliyotolewa leo Mei 12, 2023 na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF,Bw.Cliford Mario Ndimbo.

Kupitia taarifa hiyo amefafanua kuwa, "Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia maisha wanafamilia wawili kujishughulisha na mpira wa miguu.

"Mwenyekiti wa Kitayosce FC, Yusuph Kitumbo na Kocha wa mpira wa miguu Ulimboka Mwakingwe wametiwa hatiani kwa upangaji matokeo.

"Wawili hao walijihusisha na upangaji matokeo katika mechi ya Ligi ya Championship kati ya Fountain Gate FC na Kitayosce FC iliyochezwa Aprili 29, mwaka huu mjini Gairo mkoani morogoro.

"Kamati ya Maadili katika kikao chake kilichofanyika Mei 11, mwaka huu imewatia hatiani kwa kuzingatia Ibara ya 73 (9) (b) ya Kanuni za Maadili za TFF, Toleo la 2021. Kitumbo hakufika mbele ya Kamati bila kutoa udhuru wowote wa maandishi ya kupokea wito, wakati Mwakingwe aliwasilisha utetezi wake kwa njia ya maandishi. Uamuzi kamili utatolewa kwa maandishi kwa pande husika katika mashauri yao mawili,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news