Mwanajeshi ampiga risasi bosi wake, ni Waziri wa Kazi nchini Uganda

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda nchini Uganda,Kanali mstaafu Charles Okello Engola ameuawa asubuhi hii kwa kupigwa risasi na mlinzi wake nyumbani kwake Kyanja jijini Kampala.

Kanali mstaafu Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini ambapo ghafla mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbia mtaani,baadhi ya watu wanadai mlinzi huyo halikuwa hajalipwa mshahara kwa muda mrefu.

Naibu Msemaji wa Jeshi la Polisi Kampala, Luke Owoyesigire amethibitisha kisa hicho. “Ndiyo. Nenda huko Kyanja, kuna risasi. Mwanajeshi amempiga risasi bosi wake,” Owoyesigire aliwaeleza Monitor katika mahojiano kwa njia ya simu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Anita Among, pia amethibitisha kifo cha waziri huyo alipokuwa akiongoza kikao cha mashauriano leo asubuhi.

“Leo asubuhi, nilipata taarifa za kusikitisha kuwa Mheshimiwa Engola amepigwa risasi na mlinzi wake na baadaye kujipiga risasi. Roho yake ipumzike kwa amani. Huo ulikuwa mpango wa Mungu. Hatuwezi kubadilisha chochote,” Spika Among alisema.

Aidha, eneo la uhalifu limezingirwa na maafisa wa usalama. Waziri wa Jinsia, Betty Amongi ni miongoni mwa maafisa wa Serikali ambao tayari wamefika nyumbani kwa Engola huko Kyanja.(Mashirika/Monitor)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news