Polisi kujikita katika tafiti za kisayansi

NA MWANDISHI WETU

JESHI la Polisi nchini limesema kuwa katika kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia limepanga kuja na mkakati wa pamoja kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya tafiti mbalimbali ambazo zimelenga kubaini na kukomesha vitendo vya kihalifu.
Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Dkt.Lazaro Mambosasa amesema moja ya majukumu yao ni kulinda rai ana mali zao.

SACP Mambosasa amebainisha kuwa kupitia kitengo cha utafiti ndani ya jeshi hilo na katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam wameona ni vyema wafike chuoni hapo ili kujifunza masuala mbalimbali katika tafiti.

Pia amewaambia waandishi kuwam malengo ya Mkuu wa Jeshi hilo, IJP Camillus Wambura ni kuona Jeshi la Polisi linawekeza katika tafiti ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limepanga kuingia makubaliano baina ya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kufanya tafiti.

Naye Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Ralph Meela ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar Es Salaam amesema kuwa, kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia wameona ni vyema waje na mtazamo mpya katika kutanzua mbinu zinazotumiwa na wahalifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news