Rais Dkt.Samia, Museveni wazindua Mradi wa Umeme wa Kikagati-Murongo, Mbarara nchini Uganda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023. Mradi huo wa umeme utanufaisha nchi zote mbili katika masuala ya Nishati ya umeme. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Uganda mara baada ya uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati - Murongo, Mbarara nchini humo tarehe 25 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Mradi wa Umeme wa Kikagati - Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipotembelea mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo (Megawatt 16), Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.


Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati wakisikiliza maelezo ya mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news