Prof.Muhongo asisitiza Kilimo cha Umwagiliaji nchini

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara,Prof. Sospeter Muhongo ameishauri Serikali kujikita katika Kilimo cha Umwagiliaji katika kuwezesha kuleta mageuzi chanya ikiwemo kutatua tatizo la ajira, uhaba wa chakula na kuifanya sekta hiyo iweze kuchangia kwa ufanisi katika pato la taifa.
Amesema, mazao ya chakula yamekuwa ya biashara kubwa duniani. Akitolea mifano ya biashara kubwa duniani za mahindi, mchele, ngano na mihogo na hivyo ameiomba Serikali kuweka mkazo zaidi katika kilimo cha umwagiliaji likiwemo Bonde la Bugwema lililopo katika Jimbo la Musoma Vijijini.

Prof. Muhongo ameyasema hayo Mei 8, 2023 bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo.

"Wizara ya Kilimo ina umuhimu wa kufanya uchumi wetu ukue kwa haraka na iweze kitoa mchango wa ukuaji wetu kitaifa utakaotufikisha asilimia 8 hadi 10. Kwa hiyo, wizara ina jukumu la kutuhakikishia chakula kipo, ajira zinapatikana ustawi wa jamii na kuongeza pato la taifa.

"Najaribu kuweka uzito na ubunifu wanaofanya ili kilimo chetu kiweze kuwa na tija, ni lazima kwanza tuweke nguvu zote kwenye kilimo cha umwagiliaji sasa kwenye mambo ya umwagiliaji hata takwimu kutoka FAO (Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa) zinaonesha kwamba mfano mahindi, ukitumia mvua tunayoitegemea kwa hekari moja utavuna karibu tani moja mpaka tani 2.7.

"Ukienda kwenye umwagiliaji ni kati ya tani 6 hadi 9 na kule Namibia wameweza kuvuna hadi tani 11, mfano mwingine ni ngano kwa kudra za mwenyezi Mungu unapata karibu tani 4 hadi 5 kwa hekta moja, lakini ukitumia umwagiliaji unakwenda tani 8 hadi 10 kwa hiyo maboresho makubwa yaende kwenye umwagiliaji.

ZANA ZA KILIMO

"Sasa hivi duniani kuna zana nyingi za kilimo,trekta duniani sasa hivi tuna trekta milioni 16, hatujui Tanzania ziko ngapi. Lakini mfano mzuri wa Tanzania kuiga ni nchi ya India mwaka 1961, tunapata uhuru kwa hekta 1000, India ilikuwa na hekta 0.19, kwa mwaka 2000. India hiyo hiyo kwa hekta 1000, walikuwa na trekta 9, sasa hivi wana trekta 14 kwa hekta 1000.

"Kwa hiyo, Wizara ya Kilimo ipige mahesabu kwa hekta zetu tunazolima tuna hekta ngapi na India ukichukua Jimbo linalolima sana India wao kwenye hekta moja wana trekta 82. "

MATUMIZI YA MBOLEA

"Kwenye matumizi ya mbolea ikiwemo samadi wataalam wa Kilimo na Wakemia wamepiga mahesabu ukichukua tani moja ya mahindi ukalima, ukavuna unachotoa ndani ya ardhi, unachopoteza ni kilogramu 15 za Nitrogen, kilogramu 20 za potacium, kwa hiyo matumizi ya mbolea ni muhimu sana.

"Kwa hiyo hekari moja unapaswa kutumia mbolea ili uimarishe urutubisho huo unahitaji kilogramu 100 uongeze potacium oxide kilogramu 280 uongeze Phosphorus petroxide."

MBEGU BORA

"Cha nne ni mbegu bora na hii ni biashara kubwa sana duniani, Sasa hivi inagharimu karibu dola za kimarekani milioni 70, biashara ya mbegu kwa hiyo tuwekeze huko."

"Sisi Musoma Vijijini na Mkoa wa Mara kwa ujumla tunaunga mkono hoja ya bajeti. Mimi Musoma Vijijini nina mabonde mawili. Bonde la Bugwema na bonde la Suguti na Wanyere ninachoomba wale washauri waende kwa haraka tuanze kilimo cha umwagiliaji."

ASISITIZA UMUHIMU WA CHAKULA KAMA BIASHARA

"Nataka nisitize umuhimu wa chakula kama biashara kubwa duniani mfano ni kwamba mahitaji ya chakula (grobal food demands projections) mwaka 2030, tutahitaji tani bilioni 10 za chakula mwaka 2050 tutahitaji bilioni 15. Sasa kwa hiyo tutambue kwamba kilimo ni biashara."

MAHINDI

"Na chakuka mfano wa mazao ya kwanza ni mahindi, kwa mwaka 2021 wauzaji wakubwa namba moja ni Marekani amefanya biashara ya bilioni 18.8, na Ukraine amefanya biashara ya bilioni 5.8, na mwaka jana makisio ni kwamba yatahitajika mahindi tani bilioni 1.07 je Tanzania tutauza?."

"Kwa sasa hivi wazalishaji wakubwa barani Africa ni Nigeria, South Africa, Egypt, Ethiopia. Wizara ijitahidi walau ifukuzane na Nigeria kuzalisha tani karibu milioni 35.

MPUNGA

"Mfano mwingine ni mpunga asilimia 50 ya watu duniani ambao sasa hivi ni bilioni 8, wanatumia mchele kama chakula kikuu duniani.

"Na mwaka jana biashara ya mchele thamani yake ilikuwa karibu bilioni 300, na wazalishaji wakubwa ni China, mbali na kuzalisha inanunua kutoka nje. Kilimo chetu Wizara itusaidie kwenye hekta moja kama hatukupata mavuno mazuri tuvune kati ya tani 3 mpaka tani 6. Lakini tukilima kwa uzuri zaidi tufike tani 10."

NGANO

"Bashara nyingine ya Kilimo Cha mazao duniani ni ngano, kwa Sasa hivi tumo watu Bil. 8 duniani na Bil. 3 kila siku wanatumia ngano kama chakula. Biashara ya ngano ni kubwa, mwaka 2020 ilikuwa ya dola Bilioni 155, na inategemewa mwaka 2028, biashara ya ngano itafika dola Bilioni 211 ni busara kubwa sana kwa wizara kuamua kufufua na kuwekeza kwenye kilimo cha ngano.

"Wapo wauzaji wakubwa mimi nilitaka kuongelea wauzaji wakubwa hapa naomba Watanzania tutambue vizuri Egypt ananua karibu dola Bilioni 5 , Nigeria, Indonesia na Turkey karibu Bilioni 3 sasa hawa Naibu Spika, Egypt tunawapa miradi, China tumewapa miradi kumbe wananunua ngano. Kwa hiyo kumbe na sisi tuwauzie ngano turudishe rudishe kidogo."

ZAO LA MHOGO

"Zao jingine ni mhogo, biashara ya mhogo mwaka jana imetika karibu tani Mil. 280 na asilimia 70 ya mihogo duniani inazalishwa na nchi tano. Nigeria, Brazil, Tyland, Indonesia na Congo. Nigeria anazalisha kwa mwaka tani milioni 60.

"Sisi tuliombwa tupeleke mihogo China hata tani Milioni 1 hatukupata Nigeria anazalisha kwa hekari moja tani 16 je, kilimo ambacho tunafanya mabadiliko mhogo tunazalisha, tunazalisha kiasi hicho na kuvuka?."

"Hii biashara za Mhogo China anatumia dola Bil. 2.2, marekani Mil. 150, Japan Mil. 62, kwa hiyo Wizara wekeni mkazo kwenye kilimo Cha mhogo hata Musoma Vijijini nasubiria wanunuzi wapo."

MAUA

"Yani maua yaliyokatwa duniani mwaka jana hiyo biashara ukubwa wake ulikuwa Bil. 36.5, mwaka 2027 biashara hiyo ilifika karibu Bil. 45.5 angalia wazalishaji wakubwa wa maua duniani ni Netherland, Colombia, Equador.

"Nchi ya Kenya ya nne inauza maua ya Mil. 766, Ethiopia ya tano inauza maua ya Mil. 235 nimalizie kwa kusema kwamba hata sisi maua lazima tushindane na Kenya na Ethiopia ili yawe ya biashara,"amesema Prof. Muhongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news