Rais Dkt.Mwinyi aendelea kuibadilisha Zanzibar katika nyanja mbalimbali ili kuinua maisha ya wananchi

NA MWANDISHI MAALUM

NAHODHA wetu amejitolea kwa dhati kuwatumikia Wazanzibari na kuinua hali ya Zanzibar bila kujali dini, kabila na chama. 
Katika kuleta mageuzi hayo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameanza kuibadilisha Zanzibar katika nyanja mbalimbali ili kuinua maisha ya wananchi.

1. Michezo: amelenga kuimarisha sekta ya michezo kwa kuwekeza katika ujenzi wa viwanja vipya na kuboresha vya zamani, kuendeleza talanta za vijana na kuboresha mazingira ya michezo.

2. Elimu: Amejenga Skuli za Msingi na Sekondari pamoja na Vituo vya elimu jumuishi (kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum) pamoja na kuongeza mishahara ya Waalimu.

3. Afya: Ameboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya na hospitali kwa ngazi zote ikiwemo kuimarisha miundombinu ya hospitali, kutoa mafunzo ya kina kwa wafanyakazi wa afya, na kuongeza upatikanaji wa huduma za matibabu.

4. Miundombinu: kuboresha miundombinu ya barabara kuanzia barabara za ndani, Flyover, ujenzi wa Airport mpya Pemba na Unguja.

5. Uwekezaji: Ameongeza fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa Zanzibar kwa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje na kuboresha mazingira ya biashara.

6. Uvuvi: Amewawezesha wavuvi kwa kuwapa maboti yenye uwezo wa kwenda bahari kuu ambayo yana vifaa vya Gps na Fish finder vifaa ambavyo vina uwezo wa kutafuta samaki pamoja na kuwajengea diko la samaki.

7. Vituo vya wajasiriamali: amejenga vituo vya wajasiriamali kwa lengo la kuwaondoa wachuuzi kutoka mfumo genge na kuwaingiza katika mfumo soko. 

8. Uwezeshaji: Ametoa mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali wadogo wadogo na makundi mbalimbali pamoja na fursa za mafunzo ili kujiajiri na kujikimu kimaisha. 

9. Maji safi na Salama: Anapigania kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa kila mwananchi kwa kujenga matangi na kuboresha miundombinu ya maji vijijini na mijini.

10. Mishahara kwa wafanyakazi: amechukua hatua muhimu za kuimarisha hali za maisha ya wafanyakazi wa Serikali na wastaafu. 

Ni wazi kuwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameonyesha azma thabiti ya kuhakikisha maendeleo yanayomgusa kila mmoja katika jamii ya wazanzibari kupitia sera zake na mipango ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news