Rais Dkt.Mwinyi ashuhudia jambo muhimu

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo mchana ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya kuendeleza na kutangaza Zanzibar kama eneo la uwekezaji, biashara na utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Shariff Ali Shariff alitia saini kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huku Bi Elisabete Marques akisaini kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Armasite ya Qatar.

Makubaliano hayo yanalenga kuchochea ongezeko la wageni Zanzibar hasa katika sekta ya biashara na usafiri. Aidha, yatasaidia kuimarisha na kutangaza sekta ya utalii Zanzibar kimataifa. Hii inaonesha dhamira ya Zanzibar kujitokeza kama kitovu cha biashara na utalii katika eneo hilo na kote duniani.

Hatua hii inaunga mkono mpango wa Rais wenye lengo la kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya Zanzibar na Qatar.

Sasa, kuna matarajio ya kuona wawekezaji zaidi kutoka Qatar wakiwekeza Zanzibar, hatua ambayo itachangia kukuza uchumi wa nchi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news