Rais Dkt.Mwinyi ateta na Diaspora nchini Qatar

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amehitimisha ziara yake ya siku nne jijini Doha, Qatar kwa kuzungumza na baadhi ya Watanzania wanaoishi Qatar, maarufu kama wanadiaspora. 
Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Ziara yake ilijumuisha mazungumzo na viongozi wa Qatar, kusaini makubaliano muhimu, kuhudhuria Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi. 

Katika mkutano huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alijibu hoja mbalimbali zilizoulizwa na wanadiaspora hao.
Baadhi ya hoja zilizotaka ufafanuzi ni sera ya Uchumi wa Buluu,wanafunzi kupatiwa nafasi kusoma Qatar, uraia kwa watoto wanaozaliwa nje ya nchi na wazazi wawili Watanzania na pia suala la kodi wanazotozwa kwa biashara zao zilizopo Tanzania.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alizitolea ufafanuzi hoja hizo huku nyingine zikijibiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk, Balozi Mahadhi, Balozi wa Tanzania nchini Qatar na pia Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Bw. Shariff A Shariff na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Bw. Gelead Teri.
Rais Dkt.Mwinyi aliwasili Doha tarehe 21 Mei 2023 Jumapili usiku akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa tatu wa Jukwaa la Uchumi Qatar.

Post a Comment

0 Comments