Rais Dkt.Mwinyi:Serikali inaunga mkono uwekezaji katika maeneo ya uchumi wa buluu

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali inaunga mkono uwekezaji katika maeneo ya uchumi wa buluu ikiwemo usafirishaji wa baharini, mafuta na gesi, na bandari. 
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar alipotembelewa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Michael Anthony Battle kujitambulisha.

Dkt. Mwinyi amesema kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kumetokana na makubaliano yaliyofanyika baada ya uchaguzi ili kutafuta njia za kutatua tofauti zilizopo ikiwa ni pamoja na kushirikiana kuendesha na kudumisha amani na utulivu nchini. 
Naye, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Michael Anthony Battle ameridhishwa na utendaji wa Rais Dk. Mwinyi kwa utayari wake katika sekta ya biashara na uwekezaji ikizingatiwa kuwa Marekani imelenga kuwekeza zaidi nchini na kutoa fursa za ajira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news