Tanzania,Afrika Kusini kuimarisha ushirikiano kupitia utamaduni,sanaa na michezo

NA MWANDISHI WETU

UJUMBE wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu, Bw. Saidi Yakubu wamekutana na kufanya kikao cha pamoja na Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni ya Afrika Kusini na kubadilishana uzoefu ili kuboresha sekta hizo na kuwaletea maendeleo wananchi wa pande zote mbili.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya South African Heritage Resource Agency Wakili Lungisa Malgas akichangia kuhusu namna bora ya kutunza Urithi wa Ukombozi wa Afrika Kusini yakiwemo makaburi yaliyopo Tanzania Mei 26, 2023 Cape Town Afrika Kusini.

Kikao hicho kimefanyika Mei 26, 2023 katika ofisi za Wizara ya Michezo,Sanaa na Utamaduni ya Afrika Kusini jijini Pretoria ikiwa ni sehemu ya ziara ya mafunzo kwa ujumbe huo kutoka Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na timu ya Afrika Kusini juu ya namna bora ya kutunza Urithi wa Ukombozi wa Afrika Kusini yakiwemo makaburi yaliyopo Tanzania Mei 26, 2023 Cape Town Afrika Kusini. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni (sehemu ya lugha), Dkt. Resani Mnata.

Akiongea katika kikao hicho Katibu Mkuu Bw. Yakubu amewajulisha kuwa Tanzania, Uganda na Kenya kwa pamoja wanaratibu kwa pamoja michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Afcon) 2027 na kuwaomba kuunga mkono juhudi hizo za Afrika Mahariki kuandaa mashindano hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akipokea tisheti kutoka kwa Dkt. Cynthia Khumalo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni Afrika Kusini Mei 26, 2023 Pretoria Afrika Kusini.

Kwa upande wa Afrika Kusini wamesema linapokuja suala la ushirikiano, Afrika Kusini ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa kuwa udugo baina ya nchi hizo mbili ni wa kihistoria ambao umeasisiwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Nelson Mandela wa Afrika Kusini.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya South African Heritage Resource Agency, Wakili Lungisa Malgas akichangia kuhusu namna bora ya kutunza Urithi wa Ukombozi wa Afrika Kusini yakiwemo makaburi yaliyopo Tanzania Mei 26, 2023 Cape Town Afrika Kusini.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Novemba 17- Desemba 04, 2022 umekuwa mwendelezo wa uhusiano mwema kwa kuja na namna mpya ya ushirikiano kwa kuanzisha Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini na Tanzania, tamasha lililohusisha mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani na Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news