Watakiwa kujifunza kumcha Mungu

NA ADELADIUS MAKWEGA 

WAKRISTO wameambiwa kuwa wanapobatizwa wanakubali kuungama kifo na ufufuko wa Kristo, wataishi katika alama zake na huyo wanaemuamini na huyo wanaemsadiki ndiye huyo huyo anayejitambulisha kwao leo kuwa yeye ni mchungaji mwema. 
Hayo yamesemwa katika mahubiri ya Jumapili ya nne baada ya Pasaka ya Mwaka A wa Liturjia ya Kanisa, Aprili 30, 2023 katika Kanisa la Bikira Maria Mama wa Wamisionari, Parokia ya Malya , Jimbo Kuu Katoliki ya Mwanza na Paroko wa Parokia hiyo, Padri Samwel Masanja. 
“Mchungaji mwema ni yule aliyetayari kuyatoa maisha yake, akiwalinda na kuwatetea kondoo wake. Katika mazingira yetu mfano huu ni mwepesi sana kueleweka kwa sababu mazingira yetu ni ya wakulima na wafugaji, tunapozungumza habari ya mchungaji kila mmoja anaelewa ni mtu mwenye kazi gani, ni mtu mwenye jukumu gani. Mchungaji mwema ana jukumu la kuwafahamu na kuwatambua hao anawachunga, hao anaowapeleka malishoni, hao ambao amekabidhiwa. Ndugu zangu mchungaji mwema ni yule anayewangoza kondoo wake wapite katika njia iliyo sahihi.” 

Awali akisoma somo la injili ya Dominika hiyo Padri Masanja alisema, 

“Yesu aliwaambia Wayahudi, amini amini nawaambieni yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo na ukwea kwenye zizi yeye ni mwizi na mnyang’anyi, aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo, bawabu umfungulia huyo na kondoo huisikia sauti yake, naye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwapeleka nje, naye awatoapo nje kondoo wake wote huwatangulia na wale kondoo humfuta maana huijua sauti yake.” 
Misa hiyo ya pili iliyoanza saa mbili kamili ya asubuhi ikitanguliwa na misa ya kwanza iliyoanza saa kumi na mbili ya asubuhi ilisindikizwa na nyimbo zilizoimbwa na kwaya ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya (FDC) ikiambatana na maombi kadhaa mojawapo lilikuwa hili, 

“Eee Bwana Yesu, Kama mchungaji mwema, unatufungulia mlango wa kumfahamu Mungu, kabla ya kufika kwake, utusaidie kuongozwa naye katika maisha yetu, Ee Bwana.” Kwaya hii ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya ilikuwa na mwanakwaya mmoja aliyekuwa akiimba sauti ya kwanza akiwa nambali moja kwa waimbaji hao ambaye alionekana mgonjwa wakati misa hiyo ikianza huku nyimbo kadhaa za awali alishindwa kusimama na kuimba lakini baada ya muda alioneka hali yake ilitengemaa, alijisikia vizuri na kuendelea kuimba hadi misa hiyo ilipomaliza.
Mpaka misa hiyo ya pili inamalizika hali ya hewa ya eneo hili la Malya Kwimba Mwanza lilikuwa na, mawingu , manyunyu, mvua na jua kidogo kwa juma zima huku baadhi ya wakulima wakilima mahindi na mbogamboga ambazo mwandishi wa ripoti hii ameshuhudia mazao hayo yapo katika hali nzuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news