Waziri Dkt.Chana afungua Wiki ya Michezo

NA SHAMIMU NYAKI

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana jijini Dar es Salaam amefungua wiki ya michezo kuelekea Siku ya Afrika Mei 25, 2023 iliyoandaliwa na Umoja wa Wanadiplomasia wa Afrika.

Akifungua michezo hiyo Mei 21, 2023 Mhe. Chana ameisisitiza Jamii kushiriki katika michezo na mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasioambukiza pamoja na kulinda afya zao.

"Mhe. Rais Samia ameshatuelekeza kufanya mazoezi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, hivyo nasisitiza jambo hili kifanyika na kusimamia ipasavyo. Nawashukuru Wanadiplomasia Hawa kuunga mkono juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuandaa siku hii ya michezo hongereni sana," amesema.Mhe. Chana.

Bonanza hilo la michezo limeshirikisha timu za mpira wa miguu za watoto wa mabalozi, timu ya wake wa mabalozi na timu ya mabalozi dhidi ya timu ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Post a Comment

0 Comments