Serikali kujenga kituo maalumu cha magonjwa ya milipuko

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga hekari 90 kwa ajili ya ujenzi wa kituo maalumu cha magonjwa ya mlipuko (isolation center) ikiwemo ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera kutokana na mwingiliano na wananchi kutoka nchi jirani na Mkoa huo.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Mei 22, 2023 wakati akijibu swali la Mhe. Bernabetha Kasabago Mushashu katika Mkutano wa 11 kikao cha 30, Bungeni jijini Dodoma.

"Tumeshapata heka 90 ndani ya Mkoa wa Kagera kwaajili ya kujenga Isolation center itayosaidia katika matibabu ya magonjwa ya mlipuko yatayoweza kujitokeza nchini,"amesema Dkt.Mollel.

Amesema,sambamba na kujenga kituo hicho kitacho kitachosaidia kuwatenga wagonjwa wenye magonjwa ya mlipuko, Serikali itaendelea kuboresha huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa kutenga zaidi ya Bilioni 4 ili wananchi wa mkoa huo na nchi jirani waendelee kunufaika na huduma hizo.

Aidha, Dkt.Mollel amesema, kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imekamilisha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa ujenzi wa jengo la huduma za dharura (EMD) ambalo limegharimu shilingi milioni 560,000,000, jengo la uangalizi maalum (ICU) shilingi milioni 650,000,000, jengo la huduma za Mionzi (Radiology) shilingi milioni 237,000,000, nyumba ya mtumishi shilingi milioni 90,000,000.

Pamoja na hayo, Dkt. Mollel amesema, pamoja na kuboresha miundombinu katika hospitali hiyo Wizara imefanya ununuzi na ufungaji wa mashine ya CT Scan ambayo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1,810,000,000 na tayari huduma zimeanza kutolewa katika hospitali hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news