Waziri wa Afya awatoa wananchi hofu kuhusu UVIKO-19

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Afya,Mheshimiwa Ummy Mwalimu amewataka wananchi waondoe hofu kuhusu tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Uviko-19 huku akiahidi kutoa taarifa rasmi ndani ya wiki moja.

Mheshimiwa Waziri Ummy ameyaelezahayo leo Mei 14, 2023 kupitia chapisho alilobandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

"Kuhusu tetesi za uwepo wa Uviko-19. Nawaomba wananchi muondoe hofu. Tunachakata taarifa tulizokusanya kutoka hospitali na vituo mbalimbali ndani ya wiki hii tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la?.

"Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki ya tarehe 6-12 Mei 2023 watu sita kati ya 288 walithibitishwa kuwa na Corona.

"Hii ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23. Hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa na UVIKO-19.

"Wizara ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili. Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za afya na usafi.#MtuNiAfya #afyayanguwajibuwangu,"amefafanua Mheshimiwa Ummy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news