Wizara ya Madini yateta na washauri wa kodi

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali amekutana na kuzungumza na washauri wa kodi Kampuni ya PricewaterhouceCoopers Limited (PWC), Deloitte Tanzania na KPMG katika kikao kifupi kuhusu maandalizi ya Mpango Mkakati wa Miaka 10 wa Wizara ya Madini.
Aidha, kikao hiki kimefuatia maelekezo ya Mhe. Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko aliyoyatoa hivi karibuni wakati akimtambulisha Katibu Mkuu kwa watumishi wa wizara ya Madini.


Kikao hicho kimezungumzia pia kuhusu shughuli mbalimbali za uchimbaji wa madini zinazofanyika na matarajio ya Sekta ya Madini katika kipindi cha miaka 10 ijayo 
Wengine waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika leo Mei 9,2023 jijini Dar es Salaam ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Mussa Budeba, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine Ollal, Kamishna wa Msaidizi wa Madini Maruvuko Msechu, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini Tume ya Madini Venance Kasiki na Kaimu Meneja Uwekezaji na Mipango STAMICO Nsalu Nzowa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news