Yanga SC yazidi kuwa tishio

NA DIRAMAKINI

YANGA SC ambao ni mabingwa watetezi wamekata tiketi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Ni baada ya kuwachapa wenyeji Singida Big Stars 1-0 leo Mei 21, 2023 katika Uwanja wa LITI uliopo mjini Singida.

Fiston Kalala Mayele dakika ya 82 akimalizia mpira uliookolewa na kipa Benedict Haule kufuatia shuti la winga mzawa, Dennis Nkane ndiye aliyewazamisha Singida Big Stars.

Kwa ushindi huo, Yanga SC itakutana na Azam FC katika Fainali ya Azam Sports Federation Cup baadaye mwezi huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Wakati huo huo, Yanga sasa wanarejea Dar es Salaam kuanza kujiandaa na Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Aidha, wawili hao wanatarajiwa kurudiana tena Juni 3, mwaka huu huko jijini Algiers nchini Algeria baada ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kuonesha utofauti mkubwa katika msimu huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news