Baraza la Michezo Uingereza lavutiwa na maendeleo ya michezo nchini

NA ELEUTERI MANGI-WUSM 

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Uingereza Bi. Katherine Grainger ambapo amesema wamevutiwa na maendeleo ya michezo nchini.
Kikao hicho cha Viongozi hao kimefanyika Juni 27, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo wamejadili namna Tanzania na Uingereza kuimarisha ushirikiano katika michezo ambao ni wa kihistoria.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejikita katika maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika mafunzo ya michezo ambayo yametekelezwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita tangu 2012 wakati Uingereza ilipokuwa inaandaa mashindano ya Olympic ambapo walifundisha walimu wa michezo na kuhimiza watu kushiriki katika michezo.
Matokeo baada ya himizo hilo, michezo ya marathoni iliongezeka Tanzania kutoka mashindano mawili mpaka 126 ambayo yapo hadi sasa, michezo ya jogging na kuongezeka kwa idadi ya makocha ambao sasa wanafundisha ligi mbalimbali nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Uingereza Bi. Katherine Grainger amesema wataendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya michezo hasa mchezo wa Skateboard ili kuendeleza wanamichezo wa mchezo huo kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa. 
Aidha, Uongozi wa Chama cha Skateboard cha Uingereza, wapo hapa nchini kutoa mafunzo kwa kushirikiana na Chama cha Skateboard cha Tanzania ili kuimarisha na kuendeleza mchezo huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news