Dkt.Msonde atoa maagizo kwa maafisa elimu, utumishi

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI 

NAIBU Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde amewataka Maafisa Elimu na Maafisa Utumishi pamoja na watendaji wengine kuwahudumia vizuri walimu pindi wanapowasilisha changamoto zao ili zifanyiwe kazi. 
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde (kulia) akikagua moja ya miundombinu ya elimu inayojengwa katika Halmashuri ya Wilaya ya Uyui akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo.

Dkt. Msonde amesisitiza utoaji wa huduma bora kwa walimu nchini, wakati wa vikao kazi vyake na Menejimenti za Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Igunga na Nzega Mji ambavyo vililenga kuhimiza uwajibikaji na kufanya tathmini ya ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu katika Halmashauri hizo.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akikagua moja ya miundombinu ya elimu inayojengwa katika Halmashuri ya Wilaya ya Uyui akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akihimiza uwajibikaji kwa Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Nzega katika kikao kazi chake cha kuhimiza uwajibikaji na kufanya tathmini ya ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu kwenye Halmashauri hiyo.

Dkt. Msonde amesema, walimu wanalalamika kujibiwa vibaya pindi wanapowasilisha changamoto zao kwa watendaji, na kuongeza kuwa Maafisa Elimu na Maafisa Utumishi ndio wanaolalamikiwa sana kwa kutoa kauli mbaya dhidi ya walimu ambao ndio wamepewa jukumu kubwa la kulea watoto na kuwapatia ujuzi. 

“Walimu wanalalamika na kuwasilisha ushaidi wa sauti zilizorekodiwa za maafisa wote waliowajibu vibaya, ukisikiliza namna Afisa Utumishi au Afisa Elimu alivyomjibu mwalimu inaumiza sana na unaweze kutokwa na machozi hivyo wanapaswa kubadilika,” Dkt. Msonde amesisitiza. 
Baadhi ya watendaji wanaounda Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Nzega wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde wakati wa kikao kazi chake cha kuhimiza uwajibikaji na kufanya tathmini ya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu kwenye Halmashauri hiyo.

Dkt.Msonde amesema, maafisa hao wanapaswa kufahamu kuwa Mtumishi wa Umma anapaswa kutoa huduma nzuri kwa watumishi wengine na wananchi wanaofuata huduma katika maeneo yao ya kazi. 

Ameongeza kuwa, mwalimu au mtumishi yeyote akiwasilisha hoja hata kama haina mashiko asijibiwe vibaya, akitoa mfano wake mwenyewe na wa Mhe. Waziri kuwa wanapokea malalamiko ya walimu 200 hadi 300 kwa siku lakini hawatoi kauli mbaya kwa walimu hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news