Katibu Mkuu Dkt.Yonazi asisitiza ubunifu kwa maafisa habari

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amewataka maafisa habari serikalini kuendelea kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Maafisa Habari Wizara pamoja na Taasisi kutoka Zanzibar wakioongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Idara ya Habari Maelezo Tanzania Bara wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi.(Picha na OWM).

Ametoa kauli hiyo leo Juni 20, 2023 jijini Dodoma walipomtembelea katika ofisi yake kwa lengo la kuangalia na kujifunza utendaji kazi wa vitengo vya Habari, Mawasilino na Uhusiano kwa Tanzania Bara.
Ugeni huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Idara ya Habari Maelezo Tanzania Bara pamoja na Maafisa mawasiliano kutoka katika Idara ya Habari Zanzibar, wa Wizara pamoja na Taasisi zilizopo Zanzibar.

Dkt. Yonazi amesema, ipo haja ya maafisa habari kubadili mitazamo katika kuhabarisha umma kwa kuangalia mabadiliko ya kiteknolojia kwa kutumia mifumo ya kisasa inayoendana na wakati uliopo.

“Endeleeni kuwa wabunifu katika kuibua habari na si kusubiri matukio ya viongozi ndipo mhabarishe umma, hakikisheni teknolojia haiwaachi nyuma bali mnaendana nayo katika kupashana habari,”amesema Dkt. Yonazi.
Maafisa Habari Wizara pamoja na Taasisi kutoka Zanzibar wakioongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Idara ya Habari Maelezo Tanzania Bara wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi. 

Ameongezea kuwa, pamoja na kuhabarisha ni muhimu kuandika habari zinazozingatia maadili na taaluma ili kuwa na habari zinazoshi na kuufaa umma.

Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha maafisa habari kujali muda katika kutoa taarifa na vyanzo vya kuaminika ili kuepuka makosa yanayoweza kujitokeza endapo mambo hayo hayatazingatia.

“Lazima matukio na habari zitolewe kwa wakati na zenye ubora huku mkizingatia aina ya walaji wa habari hizo (audience) na kutumia njia sahihi za uwasilishaji wake,”alisisitiza Dkt. Yonazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Habari Wizara pamoja na Taasisi kutoka Zanzibar wakioongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Idara ya Habari Maelezo Tanzania Bara. 

Sambamba na hilo aliwataka kuendelea kutoa habari za serikali kwa ufanisi huku akiwasisitiza kueleza mafanikio ya miradi ya kimkakati.

Aidha, amewahimiza Maafisa habari kujifunza lugha zaidi ya moja ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya kuhabarisha umma kwani wanawafikiwa watu wengi ikiwemo wa mataifa mengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news