Rais Dkt.Mwinyi afungua ofisi za Silent Ocean nchini China

BEIJING-RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefungua rasmi ofisi za Kampuni ya Silent Ocean maarufu Simba wa Bahari, inayojishughulisha kusafirisha mizigo kutoka China kwenda Tanzania. 
Dkt.Mwinyi amesema, kuna biashara kubwa kati ya Tanzania na China na kwa kuifungua ofisi hiyo ushirikiano wa kibiashara utaongezeka zaidi baina ya nchi mbili hizo.

Pia amewahimiza wawekezaji wa China kuwekeza zaidi Zanzibar na angependa kampuni za China zije Tanzania kuangalia fursa zaidi za kuwekeza. 

Akimkaribisha Rais Dkt. Mwinyi kufungua rasmi kampuni hiyo Juni 28,2023 Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Mbelwa Kairuki amesema kufunguliwa kwa Kampuni ya Silent Ocean iwe ni chachu kwa kampuni nyingine za Tanzania kuendeleza ushirikiano wa biashara na China.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Silent Ocean,Salaah Said Mohamed amesema,wanahudumia na kupeleka mizigo kutoka China kwenda nchi zote za Afrika Mashariki na Kati kwa miaka 19 sasa.

Alibainisha uwezo wa kampuni yake kusafirisha makasha 600 hadi 1000 kwa mwezi na kupongeza uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Xi Jing Ping wa Jamhuri ya watu wa China kufungua njia ya ushirikiano kati ya China na Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news