Rais Dkt.Mwinyi aishukuru China

BEIJING-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Han Zheng.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wawili wamepongeza ushirikiano unaoendelea kushamiri baina ya Tanzania na China na Zanzibar kwa upande mmoja.

Dkt. Mwinyi ameipongeza Serikali ya China kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika miradi ya maendeleo kwa miaka 59 sasa tangu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Amebainisha, uamuzi wa hivi karibuni wa viongozi wakuu wa nchi hizi mbili Dkt. Samia Suluhu Hassan na Xi Jing Ping wa kufungua zaidi njia kuu za uhusiano umesaidia kuimarisha uhusiano.

Dkt. Mwinyi amemweleza Makamu huyo wa Rais wa China sera kuu ya Zanzibar ya uchumi na kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchi hiyo kusaidia katika uwekezaji. 

Sekta hizo ni utalii, mradi wa ujenzi wa bandari kubwa ikiwemo ya Mangapwani itakayonufaisha mataifa mengine ya Afrika, uchimbaji wa Mafuta na Gesi, uvuvi na usafiri wa baharini.
Naye Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, alimhakikishia Dkt. Mwinyi kwamba nchi yake imejizatiti kuiunga mkono Zanzibar kufikia hatua kubwa ya maendeleo ambapo amesema kwa sasa Serikali yao inawahimiza watalii wengi wa China kuitembelea Zanzibar. 

Zhang amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya maendeleo na kusema chini ya uongozi wake zanzibar imepiga hatua kubwa ya maendeleo.

Juni 29,2023 Rais Dkt. Mwinyi akiendelea na ziara ya nchini China anatazamiwa kuhudhuria Maonesho Makubwa ya tatu ya China na Afrika yaitwayo China- Africa Economic and Trade Expo katika jiji kubwa la Changsha na baadae atakuwa na mkutano maalum katika sekta ya afya utakaogusia ushirikiano mzuri uliopo wa afya baina ya Tanzania na China.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news