RC Chalamila ana kwa ana na viongozi wote wa dini kesho

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila leo Juni 6, 2023 amekutana na Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ofisini kwake Ilala Boma.
Mheshimiwa Chalamila amepata wasaa wa kuzungumza mambo mbalimbali na Viongozi hao miongoni mwa ajenda ni maandalizi ya Mkutano na Vingozi wa Dini wa madhehebu mbalimbali pamoja na chakula cha pamoja na viongozi hao wa mkoa. 

Mkutano na viongozi wa amani unatarajiwa kufanyika Juni 7, 2023 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa PSSSF- Golden Jubilee Posta.

Aidha,RC Chalamila amesema, lengo la mkutano huo na viongozi wa dini ni kuliombea Taifa pia kujitambulisha kwa Viongozi hao, ikiwa ni muendelezo wa utaratibu aliojiwekea toka ahamishiwe katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akitokea Mkoa wa Kagera.

RC Chalamila ametoa rai kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo.

Kwa upande wake Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Omary Kawambwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa amewaomba viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali kuhudhuria kwa wingi bila kukosa mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news