Prof.Muhongo ateta na wananchi Kijiji cha Muhoji

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo ametembelea Kijiji cha Muhoji Kata ya Bungwema kilichopo ndani ya jimbo hilo kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi hao.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini leo Juni 6, 2023. 

Pia, akiwa Kijijini hapo Prof. Muhongo alipata fursa ya kukagua ujenzi wa Sekondari mpya iliyopangwa kufunguliwa mwakani Januari 2024. 

Prof. Muhongo amewasihi wananchi hao kushikamana na serikali kufanikisha ujenzi wa sekondari hiyo kwa manufaa yao. 

Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuunga mkono juhudi zao ikiwemo kuleta walimu baada ya shule hiyo kufunguliwa na pia amewaomba kuzidi kutoa ushirikiano wa dhati katika suala zima la maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini na Mkoa wa Mara kwa ujumla. 

Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wamepongeza juhudi zinazofanywa na Mbunge wao Prof. Muhongo katika kuchangia ujenzi wa Sekondari hiyo ikiwemo kutoa mifuko ya saruji, nondo, mabati pamoja na kutoa hamasa kwa wananchi na wadau mbalimbali juu ya ushiriki wao katika maendeleo.

"Nichukue nafasi hii kuishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita kwa sababu hadi kufika hapa imetupa sapoti. Pia tunamshukuru Sana Mbunge wetu Prof. Muhongo kwa mara ya kwanza alipofika hapa alitoa mifuko 150 ya Saruju, lakini kwa kipindi cha pili tena ametoa mifuko 300 ya saruji, nondo 60 na mabati 110. Huyu ni kiongozi ambaye anataka maendeleo yashike kasi kisawa sawa lazima tuunge mkono juhudi hizo,"amesema mmoja wa wananchi wa Musoma Vijijini. 

Neema Nyacheri amesema kuwa, kufunguliwa kwa shule hiyo kutaleta ufanisi kwa wanafunzi katika masomo yao badala ya kutembea umbali mrefu watasoma jirani, huku pia akisisitiza wananchi kushikamana na Serikali pamoja na Mbunge wao kwa ajili ya maendeleo.

Jimbo la Musoma Vijijini lina kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374. Jimbo lina Sekondari za Kata 25 na 2 za Binafsi. Kwa sasa ujenzi wa sekondari mpya 4 unaendelea kwenye Vijiji vya Nyasaungu, Muhoji, Wanyere na Kisiwani Rukuba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news