NA ELEUTERI MANGI-WUSM
TANZANIA imeadhimisha Siku ya Yoga Duniani huku Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikisisitiza kuunga mkono sherehe za kitamaduni za mataifa mbalimbali duniani kwa sababu zinasaidia kujenga jamii ya kimataifa kuwa wamoja.
“Huu ni mwaka wa tisa sasa tangu Umoja wa Mataifa ulipotambua na kuupa mchezo wa Yoga siku maalum, Ubalozi wa India umeandaa sherehe hizi ambazo zimehuidhuriwa na watu zaidi ya 1000 kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo India na Tanzania,”amesema Bw. Yakubu.
Mchezo wa Yoga asili yake ni India unaosaidia kuufanya mwili kuwa imara kwa kupata mazoezi kuanzia kichwani hadi miguuni hatua inayofanya mwili kuwa imara na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Miongoni mwa washiriki wa maadhimisho hayo ni Balozi wa India nchini Bw. Binaya Srikanta Pradhan na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini nchini Bw. Zlatan Milišić ambapo kwa Tanzania Siku ya Yoga imeadhimishwa katika mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Arusha, Zanzibar na Kilimanjaro.
