Tanzania yazindua rasmi Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa jijini Vienna

NA MWANDISHI WETU 

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua rasmi Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini Vienna nchini Austria.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Naibu Waziri wa Austria anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal wakinyanyua mikono baada ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna, Austria.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo ni mafanikio yanayoimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Vienna na kinaonesha jinsi Tanzania inavyoipa kipaumbele Austria.
Mhe. Dkt. Tax akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna Austria.

“Kufunguliwa kwa Ubalozi huu ni mafanikio makubwa ambayo yanaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo hapa jijini Vienna na kinaonesha kwa vitendo kuwa Tanzania inaipa kipaumbele Uhusiano wake na Austria,” alisema Dkt. Tax.
Ameishukuru Serikali ya Austria na Wizara inayoshughulikia masuala ya Ulaya na uhusiano wa Kimataifa kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania Vienna tangu ulipoanzishwa hadi kufikia siku ya uzinduzi.
Kaimu Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Vienna nchini Austria Bi. Elizabeth Rwitunga akizungumza katika hafla ya kuzindua Ubalozi wa Tanzania Vienna terehe 12 Juni, 2013.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo jijini Vienna Naibu Waziri anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal amesema Austria inapongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake Austria na kuungana na nchi nyingine 16 za Afrika zenye Ubalozi nchini humo na kuahidi kuusaidia Ubalozi huo kwa kila hali ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.

“Austria inapongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake Austria na hivyo kuungana na nchi nyingine 16 za Afrika ambazo zina Balozi zao hapa nchini, niwa ahidi na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Austria iko tayari kuusaidia Ubalozi huo kwa kila hali ili ufikie malengo ya kuanzishwa kwake,”alisisitiza Waziri huyo.
Baadhi ya wanadiplomasia waliopo jijini Vienna walioshiriki hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna wakifuatilia ufunguzi huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa mataifa Vienna, Austria. Pamoja naye ni Naibu Waziri wa Austria aneyeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal ambaye alihudhuria hafla hiyo ya ufunguzi iliyofanyika tarehe 12 Juni, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa na Naibu Waziri wa Austria anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal katika picha ya pamoja na Diaspora wa Tanzania nchini Austria walioshiriki hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Vienna.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Nje).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news