Wahangaikiwe waovu nao wabadilike

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa nadra mtu kufa kwa ajili ya mtu mwovu lakini ni kawaida mtu kufa kwa ajili ya mwema, lakini kwa Kristo imewezekana maana aliweza kufa kwa ajili ya waovu, kwa hiyo Wakristo wanawajibu mkubwa wa kuwafuatilia watu waovu ili wabadilike. 
“Mimi na wewe tuna wajibu wa kuhangaika kwa ajili ya wenye dhambi, tuwashauri na kuwasindikiza katika sala zetu ili wabadilike, wajirudi na kwa kufanya hivyo taifa la Mungu litaongezeka na kuzaliwa taifa takatifu maana katika ubatizo tunatakiwa kuifanya kazi hiyo. Kazi ya kinabiii kutangaza na kuhubiri neno la Mungu, Kazi ya ukuhani kuyatakatifuza malimwengu na kazi ya uchungaji ni kuwaongoza watu kuifikia njia sahihi.” 

Hayo yamesemwa katika mahubiri ya Jumapili ya Dominika ya 11 ya mwaka A wa Liturjia ya Kanisa, Juni 18, 2023 Katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari, Parokia ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza na Padri Samwel Masanja. 
“Watu wanaohitaji kupokea ujumbe wa Mungu ni wengi, kwa hiyo tuombee miito ya Upadri, miito ya Ukatekista na miito ya Ndoa ambayo itasaidia sana kupata wachungaji na hapo ni wajibu wangu na hapo ni wajibu wetu sote tupate wachungaji wema ili kusaidia dunia kuingia katika upande tulioandaliwa sote.” 

Awali wakati wa Injili ya dominika hii Padri Samwel Masanja alisoma haya, “Yesu alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa asababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. 
"Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa Mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. 

"Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. 

"Na majina ya hao mitume ni Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea Nduguye, Yakobo wa Zebedayo na Yohane Nduguye, Filipo, na Barthomayo, Tomaso, na Mathayo Mtoza Ushuru, Yakobo wa Alfayo, na Tahdayo, Simon Mkananayo,na Yuda Iskariote ambaye ndiye aliyemsaliti.” 
Misa hiyo iliambatana na nia na maombi kadhaa mojawapo ya maombi hayo ni hili, “Uamshe ndani ya waumini wako vijana na wazee moyo wa kumfuata Mungu wako na kuifanya kazi ya utume.” 

Wakati wa matangazo ya misa hiyo umeme ulikatika huku Padri Masanja alimualika mwakilsihi maalumu kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza ambaye alifika mbele na kuomba mchango kwa ajili ya Radio Maria-Sauti ya Kikristo Nyumbani Mwako, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza linatakiwa kuchangia kiasi kinachokadilia shilingi milioni 50 kusaidia Radio hiyo ya Kanisa kufanya Uinjilishaji wa Yesu Kristo.
Kwa ujumla wakati misa hii inafanyika na kwa juma zima hali ya hewa ya eneo la Malya na viunga vyake jua ni kali lakini sasa kumekuwa na hali ya baridi kidogo ambayo inaongezeka kidogo kidogo kadili siku zinavyosonga mbele.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news