Rais Dkt.Mwinyi ateta na Watanzania wanaoishi Ujerumani

BERLIN-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema madhumuni ya ziara yake nchini Ujerumani ni kuhudhuria mwaliko wa mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu yaliyofunguliwa jana akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan. 
Ameyasema hayo leo Juni 18,2023 wakati akizungumza na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani katika ukumbi wa Hoteli ya Berlin Mariott.Rais Dkt.Mwinyi amesema uhusiano wa Tanzania na Ujerumani ni mzuri sana kwa heshima waliyotupa kutualika katika mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu.
Pia, Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali inaridhika sana na mchango wa wana Diaspora kwa maendeleo ya uchumi wa nchi kwa miamala ya fedha kwenda nchini, uwekezaji wa miradi mbalimbali. 
Amesema, Serikali imeleta mfumo wa usajili kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kwa usajili wa kidijitali kwa utambuzi pia ipo tayari kupokea ujuzi na fani mbalimbali za watanzania waliojifunza katika nchi mbalimbali kwa kujenga uchumi wa nchi.
Rais Dkt.Mwinyi amewataka wana Diaspora kuisemea vema nchi na kuwa mabalozi kwa kuzitangaza fursa mbalimbali pia amewapa moyo waendelee kufanya uwekezaji , biashara nchini Tanzania na Serikali italinda mitaji yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news