Waliojiandikisha kupata vitambulisho Desemba

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mhandisi Hamad Masauni amesema Watanzania wote waliojiandikisha na wanastahili kupata Vitambulisho vya Taifa watapata ifikapo Desemba, mwaka huu.

Ameyasema hayo Juni 14, 2023 eneo la Busisi Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza baada ya kupewa nafasi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa salamu wakati wa ziara yake ya kukagua daraja la Kigongo -Busisi mkoani hapa.

Mhandisi Masauni amesema, Serikali ilitenga bajeti ya shilingi bilioni 42.5 katika bajeti ya fedha ya 2022/23 kulipia kadi za NIDA ambazo tayari zimeanza kuja nchini na nyingine zinaendelea kutengenezwa, ambapo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan aliongeza fedha za ziada shilingi bilioni 28 kukamilisha hatua hiyo.

“Nataka kumhakikishia mbunge, wananchi wake na Watanzania wote kwa ujumla kwamba changamoto ya NIDA sasa inaenda kuisha kwa sababu tayari Rais ameshatoa fedha,

“Katika bajeti iliyopita tulitenga karibu shilingi bilioni 42.5 kwa ajili ya ununuzi wa kadi za NIDA ambapo fedha zote zimeshalipwa kadi ziko njiani na nyingine zinatengenezwa nadhani mpaka Desemba zitakuwa zimefika.

“Pia,Mheshimiwa Rais ameshatoa shilingi bilioni 28 za ziada kwa ajili ya kununua kadi, kwa hiyo tuna kadi ambazo tumeshalipa zilizotengwa katika bajeti iliyopita,tunatarajia mwezi wa Desemba kadi zote zitakuwa zimekuja na Watanzania wote ambao wanastahili kupata vitambulisho watakuwa wamepata kabla ya mwaka huu kumalizika,”amesema Mhandisi Masauni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news