Wanaswa wakisafirisha mahujaji bila kibali cha Hijja

NA DIRAMAKINI

KURUGENZI Kuu ya Pasipoti (Jawazat) nchini Saudi Arabia imewaadhibu watu kadhaa waliokamatwa wakiwasafirisha mahujaji bila kibali cha Hijja.

Hadi kufikia Dhul Hijjah 4, inayolingana na Juni 22,2023 kamati za utawala za msimu za Jawazat kwenye viingilio vya Makkah zimetoa maamuzi saba ya kiutawala kuhusiana na kutoa adhabu kwa wale waliosafirisha mahujaji wa Hijja bila kibali.

Adhabu hizo zilijumuisha kifungo cha hadi miezi sita gerezani, faini ya juu inayofikia Riyadh za Saudi Arabia (SR) 50000, kutangaza majina ya wahalifu katika vyombo vya habari vya ndani kwa gharama zao wenyewe.

Pia kufukuzwa kwa wasafirishaji ambao ni wahamiaji baada ya kutumikia kifungo na malipo ya faini na kupiga marufuku kuingia tena katika Ufalme huo kwa mujibu wa vipindi vya muda vilivyotajwa katika sheria.

Maamuzi hayo ya kiutawala pia yanajumuisha kuiomba mahakama inayohusika itoe uamuzi wake kuhusu kutaifishwa kwa gari linalotumika kwa usafirishaji ikiwa linamilikiwa na msafirishaji au mshirika wake au mbia.

"Ni vyema kutambua kwamba kamati za utawala za msimu hufanya kazi usiku kucha kutekeleza adhabu za papo hapo dhidi ya wanaokiuka kanuni na maagizo ya Hijja.

"Kamati hizi zina jukumu la kushughulikia kesi za usafirishaji haramu wa mahujaji ambao huhamishwa kutoka kwa mamlaka ya udhibiti wa uwanja.

"Wakiukaji hawa watawasilishwa mbele ya kamati, ambayo nayo itazingatia ukiukaji huo, na kutoa maamuzi ya kiutawala na adhabu dhidi ya wanaokiuka.

"Adhabu zitazidishwa na idadi ya wahalifu watakaosafirishwa,"ilifafanua Jawazat huku ikitoa wito kwa wananchi wote, wakaazi na wageni kutii sheria na kanuni za Hijja zinazotolewa na mamlaka nchini Saudi Arabia. (SG)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news