Watoto waaswa kujilinda dhidi ya ukatili mitandaoni

NA MWANDISHI WMJJWM

WATOTO wameaswa kujilinda dhidi ya ukatili mitandaoni huku wakitahadharishwa kutotumia vifaa vya kisasa vya mawasiliano bila mwongozo wa wazazi.
Hali hiyo imebainishwa na Wadau wa masuala ya kupinga ukatili wakiwemo watoto wenyewe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mkoani Dodoma Juni 16, 2023.

Wakati wa mjadala wa pamoja wa watoto na wazazi mtoto Magembe amesema baadhi ya watoto wanaotumia vifaa vya mawasiliano vya kidigitali hutumia vibaya kiasi kwamba hukutana na mambo yasiyowahusu tofauti na kujisomea kama ilivyodhamiriwa na Wazazi hivyo kufanyiwa ukatili.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Raphael Charles amesema Baraza hilo linatambua jitihada zinazofanywa na Serikali kuwalinda watoto ikiwemo kuanzishwa kwa Kamati mbalimbali za ulinzi na madawati ya jinsia.

Aidha, ameomba Serikali iendelee kushughulikia kilio cha Watoto dhidi ya ukatili wa mitandaoni kwa kuwachukulia hatua stahiki wale wote wanao wafanyia ukatili. Vilevile, ameomba jamii nayo itoe ushirikiano kwa vyombo vya dola pale ukatili unapotokea kwa watoto. Hata hivyo amesema watoto pia wana wajibu wa kutoa taarifa wanapofanyiwa ukatili.
Awali akitoa salaam za Wizara Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesistiza jamii pamoja na Wadau kuendelea kupinga ukatili dhidi ya watoto hasa ukatili wa mitandaoni.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Watoto (UNICEF), John George amesema jamii ina wajibu wa kuhakikisha mitandao ya kijamii inatumika kwa manufaa mazuri, huku akionya jamii kuacha kusambaza taarifa zao binafsi kwenye Mitandao.

Akitoa hotuba yake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema utafiti uliofanywa na Wizara l pamoja na UNICEF mwaka 2022 ulibainisha 67% ya watoto wenye umri kati ya miaka 12 hadi 17 wanatumia simu; na kwamba asilimia 4 kati yao wamefanyiwa ukatili.

Ametoa rai kwa wazazi, walezi na jamii kuwajibika katika malezi, makuzi, matunzo na ulinzi wa watoto ili kuwezesha kuwa salama.
Katika maadhimisho hayo, Waziri Dkt. Gwajima amezindua mwongozo wa kupinga ukatili wa watoto kwenye michezo, vitini vya mafunzo ya malezi ya watoto na Baraza la watoto Taifa. Aidha, ametoa vyeti kutambua mchango wa waliojitolea kuunga mkono Kampeni ya kupinga ukatili kwa akiwemo Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Sospeter Bulugu na Wenyeviti wa SMAUJATA wa Mikoa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news