Waziri Balozi Dkt.Chana akagua ujenzi jengo la wizara

NA SHAMIMU NYAKI

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Juni 8, 2023 amekagua ujenzi wa Jengo la wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma na kuridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika jengo hilo.
Mhe. Chana amemtaka Mkadarasi wa Jengo hilo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi ujenzi huo ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Naye Mhandisi wa Jengo hilo Bw. Omari Saidi amesema kuwa wanahakikisha jengo hilo linaendelea kujengwa kwa viwango, kasi na kuahidi kulikabidhi Oktoba mwaka huu 2023 kama Mkataba unavyosema.
Awali Mhe. Chana alitembelea eneo la Ujenzi wa Uwanja wa Dodoma ambapo ameshuhudia baadhi ya vifaa vya ujenzi vikiwa tayari katika eneo hilo kuanza ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news