Yanga SC yafa kiume Kombe la Shirikisho

NA DIRAMAKINI

MECHI ya Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na USM Alger ya nchini Algeria imetamatika kwa Watanzania hao kushindwa kufikia lengo la kutwaa ubingwa, licha ya kuonesha kandanda safi ugenini.

Ni kupitia mtanage ambao umepigwa usiku wa Juni 3, 2023 kuamkia Juni 4, 2023 katika dimba la Stade du 5 Juillet jijini Algers.

Yanga SC wameshindwa kutwaa taji hilo baada ya ushindi wa Aggregate ya mabao 2-2 ambapo, awali USM Alger iliwachapa mabao 2-1 Yanga katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku mtanage wa leo Yanga wakiibuka kidedea kwa bao moja.

Bao la leo la Yanga SC limefungwa na Djuma Shabani dakika ya 7 kwa penalti baada ya Fiston Mayele kuangushwa kwenye boksi ya kipindi cha kwanza ambalo lilidumu kipindi chote cha mtanange huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news