Dar yawatoa hofu wananchi kuhusu vifaa tiba vilivyodaiwa kusafishwa na kuanikwa Kivule

DAR-ES-SALAAM (Julai 7,2023)-Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Saaam anaomba kutoa Ufafanuzi juu ya video fupi inayosambaa katika Mitandao ya Kijamii leo tarehe 07 Julai,2023. 
Video hii imerekodiwa ikimuonyesha Mtumishi ambaye ametambulika kwa jina la Ndugu Deborah Chacha (Mtumishi wa usafi) aliyekuwa amepewa jukumu la kuchambua na kusafisha vifaa tiba vilivyokuwa vimehifadhiwa stoo, lengo la Uchambuzi likiwa ni kutambua vifaa vinavyoweza kutumika na visivyofaa viweze kuondolewa.
Mtumishi huyu alionekana nje ya jengo la Wazazi akichambua, kusafisha na kuanika vyombo hivyo katika ngazi moja ya jengo la hospitali, hali iliyoleta taharuki kwa wananchi na kutoa taswira kwamba vifaa hivyo ndio vinavyotumika kwa wagonjwa katika matibabu yao.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam anapenda kuutarifu umma na kukanusha kuwa taarifa zilizorekodiwa na kusambazwa hazina ukweli wowote na kwamba vifaa tiba hivyo havikuwa vimetumiwa na wagonjwa na kwamba ni vifaa vilivyotolewa stoo ili kuchambuliwa kubaini vifaa tiba vinavyofaa na visivyofaa kwa matumizi.
Vifaa vvyote ambavyo huandaliwa kwa ajili ya huduma, hupitia utaratibu wa kuvitakasa kwanza kitaalamu kwa kutumia mashine na mitambo ya utakasaji (disinfection and high Temperature Sterilization) kabla ya kutumika kumuhudumia mgonjwa ili kuhakikisha usafi na kutoambukiza vijidudu vya Magonjwa kwa mgonjwa, hivyo vifaa vilivyotoka stoo baada ya uchambuzi vitakavyo faa vitapitia utaratibu huu wa kitaaluma kabla ya matumizi kwa mgonjwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news