Naibu Wakili Mkuu:Kamati ya Ukaguzi ni jicho la taasisi ifanye kazi kwa uhuru

NA MWANDISHI OWMS

NAIBU Wakili Mkuu wa Serikali,Bi.Sarah Mwaipopo amefungua mafunzo ya kujenga uelewa kwa wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) kuhusu majukumu ya Kamati ya Ukaguzi.

Mwaipopo amefungua mafunzo hayo mkoani Morogoro yanayofanyika kwa siku mbili kwa wajumbe wa kamati hiyo ili kuhakikisha kuwa Kamati inaifahamu taasisi ili kuweza kumshauri Afisa Masuuli na wajumbe wa Menejimenti ili kuweza kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ambapo amesema kuwa kamati hiyo ni jicho la taasisi.

‘’Kamati ya Ukaguzi ni jicho la taasisi na chombo muhimu katika uendeshaji wa taasisi ili kuhakikisha kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za Serikali na Kamati ifanye kazi kwa uhuru, Menejimenti ya OWMS iiwezeshe Kamati ya Ukaguzi kutekeleza majukumu yake kuwa na uelewa wa pamoja na kushirikiana,’’amefafanua Mwaipopo.

Pia, ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi na wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kupata uelewa wa majukumu ya Kamati ya Ukaguzi; mahusiano baina majukumu ya Kamati ya Ukaguzi na Menejimenti, majukumu ya Mkaguzi wa Nje na ya Mkaguzi wa Ndani ikiwemo kupata uelewa ili kuweza kusimamia na kudhibiti vihatarishi.

Mwaipopo ameipongeza Kamati ya Ukaguzi kwa kazi nzuri inayofanya ya kuisimamia na kushauri OWMS katika uendeshaji wa taasisi na inaiwezesha OWMS kupata hati safi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa OWMS, Dkt. Omari Fadhil amemshukuru Mwaipopo kwa kuona umuhimu wa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika.

"Na kwa niaba ya kamati tutaendelea kukupa ushirikiano ili OWMS iendelee kupata hati safi na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, taratibu na na kanuni na tutoe ushirikiano kwa Mkaguzi wa Nje, Mkaguzi wa Ndani na Kamati ya Ukaguzi."

Mafunzo yanatolewa na Dkt.Mwamba Jingu, Mkufunzi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha na yanaratibiwa na Joan John, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Ofisi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news